wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, June 06, 2009

TweetThis! Kama fisadi, ni fisadi, huo si ubaguzi wa rangi - Mohamed Raza

Akizungumza na gazeti Raia Mwema alisema:

Mtu utahukumiwa kwa matendo yako kama ni mwizi utaitwa mwizi na kama ni fisadi utaitwa fisadi hakuna cha ubaguzi wa rangi hapa…tusipotoshe watu. Matendo yenu ndiyo yanayotumiwa na wananchi kuwahukumu.

Leo hii utasikia au kuona baadhi ya viongozi wanashindwa kutembea mitaani mchana kwa kuhofia kuzomewa kuwa ni mafisadi…wengine wakitajwa wanajidai kuwa huo ni ubaguzi wa rangi…mimi nasema hakuna ubaguzi wa rangi katika suala la ubadhirifu.

Wizi unatisha serikalini tena ukihusisha baadhi ya viongozi…zamani CCM ilikuwa haitaki mchezo wa namna hiyo na yeyote anayehusika hatua zilichukuliwa hata kama kiongozi anatuhumiwa tu, aliwekwa kwanza nje ya uongozi wa chama na serikali ili kupisha uchunguzi

Lakini leo hii hili halifanyiki ndani ya CCM wapo viongozi watuhumiwa lakini wameachwa hawajasimamishwa, sisemi kwamba wana makosa moja kwa moja lakini kama mtu unatuhumiwa na kama unakipenda chama chako na huna shaka yoyote na huna uroho wa madaraka kwa nini usikae pembeni kupisha uchunguzi?

Anahoji: Iko wapi CCM ya mwaka 1977 iliyozaliwa baada ya kuunganishwa kwa vyama vyenye uadilifu na uzelando wa TANU na ASP?

Analaumu: ....wasaidizi wa kiongozi huyo mkuu wa nchi, akiamini kuwa hawezi kufanya mambo yote mazuri kwa nchi peke yake bila mwongozo mzuri na bora kutoka kwa wasaidizi wake.
Kwanza, Rais ameonyesha utayari mkubwa wa kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote na ndiyo maana leo tunaweza kuzungumza hivi lakini utayari huu wa Rais unaonekana kupingwa kwa chini chini na baadhi ya wasaidizi wake. Kuna hali ya kulindana kuanzia katika chama hadi serikalini na taasisi nyingine.
Kama chama kingekuwa kinamuunga mkono Rais bila shaka yoyote ni lazima watuhumiwa wengine wenye nyadhifa na ambao bado wako katika chama kama viongozi wangesimamishwa kwanza kupisha uchunguzi na kama watabainika safi warejeshwe huu ndiyo utaratibu bora wa chama bora au serikali bora.

Anasikitishwa: ....na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, na hasa suala la kuporomoka kwa maadili.

Anatonya na kuonya: Kuna mchele unatolewa na Japan ambao utauzwa kwa wafanyabiashara ni kweli kila mfanyabiashara anataka faida lakini malengo ya mchele huo yasiharibiwe wananchi wauziwe kwa bei nafuu, mchele huu usiingie mikononi mwa mafisadi.
Chakula kilicholetwa na Serikali ya Japan, kwa ajili ya kuuzwa kwa wafanyabiashara kwa bei nafuu ili nao wawauzie wananchi kisiachwe kiwafikie mafisadi kwa kuwa watawalangua wananchi na hasa ikizingatiwa kuwa matendo yao yanathibitisha kuwa hawana huruma kwa wananchi masikini.

Mohamed Raza alikuwa mshauri wa masuala ya michezo wa aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar Dk. Salmin Amour

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads