wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, May 05, 2009

TweetThis! Rostam awasilisha tuhuma TAKUKURU dhidi ya Mengi

MBUNGE wa Igunga, Rostam Azizi,jana alitimiza ahadi yake baada ya kupeleka vielelezo anavyodai vinahusu tuhuma za ufisadi dhidi ya mfanyabiashara Reginald Mengi na kutangaza rasmi kufunga mjadala wa suala hilo.

Rostam, ambaye Jumapili alimlipua Mengi akimwita nyangumi wa ufisadi baada ya mwenyekiti huyo wa IPP kumtaja katika orodha ya watu watano aliodai kuwa ni mafisadi papa wanaoifilisi nchi, aliahidi kuwasilisha vielelezo hivyo kwenye vyombo vya dola ili vianze kumchunguza Mengi.

Jana jijini Dares Salaam, mnamo saa 10:15 jioni, Rostam alitimiza ahadi hiyo kwa kukabidhi vielelezo hivyo kwenye ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ambako vilipokelewa mmoja wa maofisa taasisi hiyo.

Miongoni mwa tuhuma ambazo Rostam alimrushia Mengi ni pamoja na kuuruka mkopo wa karibu Sh5 bilioni ambazo zililipwa kwa kampuni ya Anche Mwedu inayomilikiwa na mfanyabiashara huyo na ambazo ukichanganya na riba yake hadi kufikia sasa ni Sh28 bilioni.

Kashfa nyingine ni pamoja na kuilazimisha kampuni ya uwekezaji ya Nico kununua kiwanda cha Interchem kinachomilikiwa na kaka wa Mengi, wakati akijua kuwa kilikuwa kinakaribia kufa.

Baada ya kuwasilisha vielelezo hivyo, Rostam alisema asingependa tena kuendeleza mjadala huo kwani ameshaufunga kwa kutoa vielelezo hivyo kama alivyoahidi.

"Nimetimiza ahadi yangu. Niliahidi kutoa vielelezo wakati wa mkutano wangu na waandishi wa habari na sasa nimetimiza. Mjadala na yeyote mwenye chohote dhidi yangu apeleke kwenye vyombo vya sheria si kutuhumu," alisema Rostam, ambaye kama Mengi anamiliki vyombo vya habari.

Alisema huu si wakati wa watu kutuhumiana tena kwa vyombo vya habari, bali njia nyepesi ni mtu mwenye ushahidi kuwasilisha vielelezo hivyo katika vyombo vya dola.

Naye ofisa uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema kama ilivyo kawaida, kwa kutumia kifungu cha 11, tuhuma hizo zimechukuliwa kama zinazowasilishwa na raia wengine wa kawaida kisha kufanyiwa kazi.

"Tumezipokea, tutazifanyia kazi kama tuhuma nyingine zinazotolewa na raia yeyote hatusemi kuhusu uchunguzi kwani kifungu cha 37 kinakataza hilo," alisema Kapwani.

Katika hatua nyingine, Leon Bahati anaripoti kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema kuwa hadi jana wizara yake ilikuwa haijapata vielelezo vinavyohusiana na tuhuma dhidi ya Mengi, ambaye Rostam alidai kuwa kampuni zake zinakwepa kodi.

Naye Boniface Meena anaripoti kuwa mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo amesema malumbano ya Mengi na Rostam hayaisaidii nchi na kuwataka waache kuvuana nguo kwa mambo yasiyo na msingi.

Naye Salim Said, anaripoti kuwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislaam wameitaka serikali kuingilia kati malumbano yanayoendelezwa na wafanyabiashara hao wawili kwenye vyombo vya habari - Ramadhan Semtawa,  Mwananchi

6 feedback :

Anonymous said... Tue May 05, 02:45:00 PM MST  

ni sawa na mzazi kuendelea kuwasikiliza watoto wako wawili wakigombana bila kuingilia kati. SASA BASI, TUNAOMBA KUSIKIA TAMKO LA RAISI KUHUSU HILI

Anonymous said... Tue May 05, 02:54:00 PM MST  

jamani naomba wasomaji mnisahihishe, kweli tunakubali kufanywa kichwa cha wenda wazimu ambapo Mengi na Rostam wanajifunzia kunyoa? ni sawa na watu wanabishana kuwa jana ulikula maini ya kukaanga na mwingine no ulikula kuku wa kuchoma wakati sisi hata hayo matembere hatuna uhakika wa kuyapata. NAWAHAMASISHA WANANCHI HEBU TUAMKE, TUWAPELEKE HAWA WATU MAHAKAMANI WAKAYATOE HAYO MADAI YAO ILI TUJUUE UKWELI KAMA UKWELI WA AKINA ZOMBE.

Anonymous said... Tue May 05, 08:36:00 PM MST  

mimi binafsi naona kuna umuhimu tena wa makusudi kabisa kujaribu kuhusisha serikali kuu na haya malumbano tena kuilazimisha kufanya kazi yake na si kwa wao kukemea kuwa watu wakae kimya bali kuangalia ukweli wa yale yanayotamka, kinachotakiwa sasa hivi ni kwa rostam na Mengi wote kuwakilisha vielelezo vyao mbele ya sheria na kujibu shutuma dhidi yao. Sidhani kama wote ni wasafi lakini nachoona hapa kuna makosa makubwa makubwa ambayo serikali kwa namna moja ama nyingine inahusika na kinachofanyika sasa hivi ni serikali inahaha kutafuta namna namna ya kuwanyamizisha hawa wote wawili kabla mambo hayajaharibika kabisa.
Naisikitia sana nchi yangu najua ndio basi tena imeshauzwa. Nashukuru nilizaliwa Tanzania na nashukuru kwa yote iliyonifanyia lakini siwezi kuangalia watoto wangu wakizaliwa kwenye nchi isiyo na mwelekeo kila mtu anajifanyia anachojua, kila mtu anapopata nafasi anaiba basi hakuna kuangalia kizazi kijacho kitakulia wapi wala kitasoma nini.
Ubinafsi na ulafi umeiua Tanzania yetu.

Subi said... Tue May 05, 08:59:00 PM MST  

Kwa kweli kinachosikitisha zaidi kwa sasa ni vile ambavyo wakuu wa mamlaka wamekuwa kimya kama vile kuashiria aidha wanaopambana wakichoka watakaa kimya na wananchi watasahau au wanahusika kwa namna yoyote iwayo katika hii sakata hivyo wanakoka mbinu za kujiweka mbali ama wanakusanya uthibitisho kabla ya kutoa tamko na hatua madhubuti.
Hali ilivyo kwa kweli inatakikana jambo la maana sana lifanyike kurudisha imani ya wafuatiliaji wa mambo.

Mzee wa Changamoto said... Wed May 06, 07:17:00 PM MST  

Kwa kuwa naandaa kitu kuhusu hili huku shamba, wacha niendelee. Asante Da Subi kwa hii. Imekaa vema

Bady said... Sat May 09, 08:41:00 PM MST  

Rostam akatae kwa njia teyote yeye ni FISADI na hao wenzake wa nne waliobaki, Rostam kahusishwa na DOWANS,Rostam kahusishwa na KAGODA,Rostam kahusishwa na RICHMOND,Rostam asifikiri watu wanapokuwa kimya hawana uchungu na nchi yao, Rostam amekuwa nani?,anatuhumiwa na WABUNGE wengi ndani ya BUNGE tena wakiwa ni wabunge wa CCM,alijiingiza ktk malumbano na Mh MWAKYEMBE kwa uchafu alio nao mpaka akafananishwa na MAJI TAKA, tunamwambia asifikri sisi ni wajinga kwa kuegemea kivuli cha UDINI,UBAGUZI WA RANGI, na mengine anayoona kwa mtizamo wake finyu kuwa ndiyo sababu.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads