wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, April 16, 2009

TweetThis! Umuhimu wa kusikiliza na kuwa makini katika mawasiliano

Mgonjwa mmoja mahututi asiyeweza kusema na kuwekewa oxgen alikuwa anaombewa na Mchungaji. Akiwa anaombewa, mgonjwa alichukua kalamu na karatasi na kuandika kisha kumpa Mchungaji aliyekuwa akimwombea. Mchungaji aliitia mfukoni ile karatasi badala ya kuisoma kwanza na kisha akaendelea na maombi na kwa bahati mbaya mgonjwa akakata roho katikati ya maombi.

Mchungaji hakuisoma ile karatasi kwa kuwa alijua ni wosia wa marehemu ndipo akasubiri hadi baada ya maziko na kisha kwenye kikao cha ndugu akasema; "Kuna kitu nilipewa na marehemu siku nilipokuwa nikimuombea".
Ndipo akampa mmoja wa wanandugu asome. Hiiki ndicho kilichokuwa kimeandikwa na marehemu: "Mchungaji, UMEKANYAGA WAYA WA OKSIJENI, NAKOSA HEWA".

5 feedback :

Subi said... Fri Apr 17, 02:16:00 AM MST  

Ha ha haa, Mama Malaika, nami nilisema sentensi inayofanana na hiyo, 'kamata huyo mchungaji, chapa fimbo huyo, kaua ndugu yetu' ha ha haa

MAKULILO, Jr. said... Fri Apr 17, 04:04:00 AM MST  

Da Subi,Mi naona hapo mchungaji hata kama asipopelekwa polisi na kutiwa ndani, au kulambwa mboko na mkuu wa wilaya wa Dot.Kanyigo (Bukoba), naamini kabisa nafsi ya mchungaji huwa ilikua inamuuma sana kwa technical mistake ile aliyoifanya ya kutosoma ujumbe ule muhimu sana.Naamini hapo wanandugu lazima walimpa kichapo tu, Tuendelezee Da Subi iliendeleaje ktk kikao hicho??Kitu kingine, najua huyu mchungaji aliduwaa sana na kupatwa na mshtuko mkubwa baada ya kusoma ujumbe huo.Na kwa bahati mbaya mchungaji hakua amesoma ujumbe ule kabla kutokana na ubize.MAKULILO, Jr.www.makulilo.blogspot.com

Kennedytz said... Fri Apr 17, 06:08:00 AM MST  

Subi mambo, hilo ndio tatizo la kibinaadamu leo yeye kesho sisi
Pia kuna usemi kwamba "kabla ujatoa boliti kwenye jicho lake toa kwako kwanza"
Sisi wana wa-adamu tunajua matokeo lakini, hatujui sukunde inayofuata kutakuwaje!
Pia tunapenda kuhukumu kuliko kuhukumiwa
Kumbuka Subi kila kitu kina sababu yake na kifo cha huyo mgonjwa kimemtokea
huyo mchungaji.
Yuda alimsaliti Yesu kwa fedha, na Petro alimkana pia. Lakini kwa kifo chake
wote tumesamehewa na kuzaliwa upya katika maisha haya
Bsai Mchungaji, akukusudia kumuua huyo mgonjwa ila hakuna anayejua kwanini ilitokea hivyo
Subi nimesikia unaitwa Mama Malaika, mhnnnn jina zuri sana subi

Subi said... Fri Apr 17, 07:02:00 AM MST  

Makulilo, ha ha haa, unanitaka ugomvi na ndugu wa marehemu, ha ha haa, kilichoendelea hapo ni kukisia tu ha haa, pengine mkong'oto na mbata na kabali za kukaribia kutoa roho ha ha ha (utani).
 
Kennedy, mi si Mama Malaika ila Mama Malaika ndiye ameacha maoni nami nikamjibu!
Nimesoma ujumbe wako na kuuelewa, huenda ipo sababu ya marehemu kufa lakini hatujui maana yake chetu kilio ni kumpoteza mwenzetu kwa ubize wa Mchungaji na sala (pengine zilizomwingiza marehemu kuzuri zaidi).
 
BTW: Kenny asante kwa habari za Magazetini.

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads