wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, April 27, 2009

TweetThis! Kashangae feri ya Bongo

Mdau mmoja wa kundi pepe fulani katuma hizi picha za hiki chombo cha safari za majini akaniambia nikashangae feri maana ndo lipo katika bahari ya hindi Bandari ya Salama alias Bongo au Daslam.

Mi nikajiuliza sijui hilo gudulia hapo limefunika herufi "E"? ama hicho chombo ni cha kitalii toka Asia ambako wana asili ya majina kama hayo ama ndo kimenunuliwa hakijabadilishwa jina ama ndo kimojawapo cha yaliyokamatwa kwenye wizi wa samaki wetu? au pengine tu ni chombo kama chombo kingine cha usafiri cha mmiliki wa kawaida tu Bongo anafanya zake shughuli za usafiri, isije ikawa taabu tena, manake mtu akiumwa na nyoka basi siku akiona jani kavu atatimua mbio na mawenge bila sababu na akaanza kusema hovyo bure.

1 feedback :

MAKULILO Jr, said... Mon Apr 27, 01:52:00 PM MST  

Da Subi,
Inabidi tuondoe hilo gudulia tupate uhakika.Isijekuwa na la Mh wetu.Na kama ni mtu ametumia jina la mh bila idhini yake tutajua tu, au kama ana ubia nao tutajua tu.Ila nimekubali mambo ya gudulia.

Asante kwa picha hii

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads