wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Tuesday, March 17, 2009

TweetThis! Majaribio ya mbinu nyingine ya wizi Tanzania

Ugumu wa maisha ndiyo unaosababisha watu wafanye viroja visivyotarajiwa katika dunia ya sasa. Ni dhahiri kuwa kila tuonapo mawio, binadamu yeyote mwenye afya na uwezo wa kufanya kazi inampasa kutimiza wajibu wake wa siku. Mara nyingi hatuna uchaguzi bali kujituma ili kuweza kukidhi mahitaji muhimu ya kibinadamu na pengine kwa ajili pia ya ndugu na jamaa zetu.
Anayeonekana katika picha hapo akiwa ndani ya boksi ni mtu anayetuhumiwa wizi baada ya kufichwa kama mzigo na wenzie katika harakati za kumwingiza kwenye duka moja la kuuza bidhaa za jumla. Lengo la mbinu hiyo ilikuwa ni kufanikisha wizi wa fedha kutoka kwenye duka hilo pale ambapo saa za kazi zingetimu na duka kufungwa. Kama wakale walivyoasa ya kuwa, za mwizi thelathini na tisa na ya arobaini hukamatwa, mwenye duka 'alichezwa chale' alipoliona boksi, hivyo akawaamuru waliokuwa wamelibeba 'boksi' hilo kulishusha chini na kisha walifungue. Kauli hiyo ilisababisha kimbembe ambapo, watu waliokuwa wamelibeba boksi hilo walitimua mbio kila mmoja kushika njia yake bila ya kujali kuwa hawakumweka huru mwenzao ili naye ajiunge nao katika mbio hizo. Hatima yake ni suluba ya kipigo kilichomfika pasina huruma.

Kisa hiki cha kweli kimetokea huko mjini Mwanjelwa mkoani Mbeya.

Swali la kujiuliza, ni je, msingi mkuu wa kujiajiri katika dunia ya leo, yaani elimu, unafanya kazi katika kumwandaa mwananchi wa sasa kupambana na hali za maisha katika ulimwengu huu wa ajira binafsi?

Picha ni kwa hisani ya Mpoki Bukuku (Mzee wa Sumo) mwenye Blogu ya Wananchi

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads