wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, February 28, 2009

TweetThis! Tanzania vs Zambia LIVE online [updated]

  • Zambia wanasonga mbele katika nusu fainali ya CHAN.
  • Mpaka datika 90(+6) zinakwisha matokeo ni Tanzania 1 Zambia 1.
  • Dennis Banda anaipatia Zambia bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi baada ya kupokea krosi ya kona iliyopigwa na Stanley Banda.
  • Kocha wa Zambia anasema haina haja ya kucheza dakika tano za majeruhi anadai penati iliyotolewa ilikuwa zawadi kwa Tanzania hivyo mechi iishe tu.
  • Shadrack Nsajigwa ameipatia Tanzania bao kipindi cha pili kwa njia ya penati baada ya mabeki wa Zambia kufanya uzembe langoni pao walipokuwa wanaokoa mpira. Mmoja wa mabeki alipiga mpira kuutoa nje na mwenzie aliyekuwa ameketi kwenye mstari (Davy Kaumbwa) akaugusa kwa mkono, refa akatoa penati na kadi ya njano kwa mchezaji mwingine wa Zambia aliyemsukuma refa.
  • Hadi mapumziko dk. 45 za kwanza, mabao ni 0 - 0.
  • Tanzania inahitaji kushinda ili iweze kusonga mbele, matokeo yakiwa droo, Zambia itasonga mbele.

2 feedback :

Matiya said... Sat Feb 28, 11:35:00 AM MST  

Hongera sana dada Subi,kupitia blog yako umetuwesha hata sisi tulioko ughaibuni kutizama mechi live kwenye laptop zetu. Keep it up!

Mzee wa Changamoto said... Sat Feb 28, 07:34:00 PM MST  

Da Subi. Asante kwa mara ya tena.
Nimeimiss hii mechi kidogo lakini nimepata updates zako. Hivi umesema una uchu na taifa Stars? Ya kweli hayo? Lol. Just kidding
Nakutakia wikiendi njema na kazi njema pia.
Blessings

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads