wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Wednesday, January 28, 2009

TweetThis! Tangazo la blogu mpya 'matondo.blogspot.com'

Mnakaribishwa katika blogu mpya ya 'matondo'
CHAKULA KITAMU NA KICHUNGU VYOTE VINAWEZA KUMFANYA MLAJI AKAKUNJA USO
Ni lini ulisoma kitabu kipya ukakimaliza? Ni lini ulifikiria jambo kwa kina ukalichanganua na kupendekeza masuluhisho kadhaa mbadala? Ni lini ulipochangia mjadala kwa kutoa hoja nzito zenye mashiko? Mbona tumebakia kuwa washangiliaji tu - tena wa falsafa na nadharia kongwe zilizochakaa na kujaa maluweluwe? Fikra mpya ziko wapi katika jamii? Tunakoelekea ndiko? Blogu hii ni kwa watu wanaopenda kufikiri na itajishughulisha na uchambuzi na uchanganuzi wa mambo mbalimbali kwa kina.
Hayo ni maneno yanayobeba maudhui yaliyomo katika wa blogu mpya ya 'matondo'.
Kwa heshima kubwa na taadhima tele nabisha hodi tena kwenu mliotangulia. Naomba mnifungulie mlango na kunikaribisha tena. Safari hii nakuja na blogu ya kuchangamsha fikra na uchambuzi. Blogu hiyo inapatikana hapa www.matondo.blogspot.com
Natanguliza shukrani zangu kwani najua mmeshanikaribisha.

Wenu;
Dr. Masangu Matondo Nzuzullima
Chuo Kikuu cha Florida

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads