wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, January 17, 2009

TweetThis! Audio - Kalembe Ndile apeleka TV ili Mawaziri watizame Obama akiapishwa wakiwa Kenya

Kumekuwepo ripoti kuwa nchi ya Kenya inatuma ujumbe wa watu kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kushuhudia na kushiriki sherehe za maapisho ya Raisi wa nne wa Marekani bwana Barack Obama hapo Januari 21. Inafahamika kuwa asili ya Barack Obama ni Luo, Kenya kwa upande wa baba yake na hivi Wananchi wengi wa Kenya na WaAfrika wengi wanajivunia kwa hili.

Lakini, wapo wale wanaoshindwa kupata maana halisi ya Serikali ya Kenya kugharimia safari ya hii ikiwa Wananchi wake wanateseka kwa njaa na hasa baada ya Raisi wa nchi bwana Mwai Kibaki kutangaza kuwa nchi hiyo imekubwa na baa la njaa na hivyo inahitaji msaada wa hali na mali usiopungua takriban fedha za Kenya Shilingi bilioni thelathini ili kukabiliana na baa hilo. Mmoja wao ni Bwana aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Utalii nchini Kenya bwana Kalembe Ndile.
...unajua kwanza ni lazima WaKenya waelewe kuwa huyu ni Raisi wa Marekani, hata kama alitoka Kenya, saa hii ataangalia mambo ya Marekani kwanza!
...waende na pesa zao, wasiende na pesa za umma.
...kwa sababu hawajaalikwa, wanaenda kujiingiza tu huko.
...kwa sababu tuna baa la njaa, kwa hivyo sioni vile wanaweza kutumia pesa mingi hivi waende wakaangalie runinga! kwa rooms zao! si wangeangalilia runinga hapa! ...
Mwandishi wa habari wa BBC Swahili wa Kenya bi Carolyne Karobya alizungumza na bwana Ndile aliyebeba Televisheni na kuitoa kama zawadi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ili iwe msaada kwa viongozi hao kuitizama. Bwana Ndile anashindwa kuelewa ni kwa nini Viongozi wakaangalizie TV Marekani ndani ya vyumba badala ya kubaki Kenya na kuitizama wakiwa majumbani mwao.

Ifahamike kuwa Viongozi hawa baadhi yao walinyimwa viza za kwenda Marekani. Wale waliobahatika vile vile hawajaalikwa katika sherehe hizo na wala hawataruhusiwa kuhudhuria maadhimisho siku hiyo katika viwanja ya Washingon, Marekani.

Msikilize bwana Kalembe Ndile:

Kalembe Ndile of Kenya recorded from BBC Swahili by Subi

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads