wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Monday, December 01, 2008

TweetThis! "Ukaguzi wa majengo Benki Kuu ni usanii mwingine"

Nimepokea habari hii toka kwa msomaji wa blogu, ipo hivi:

UKAGUZI WA MAJENGO BENKI KUU NI USANII MWINGINE

Jamani usanii umetuzidi watanzania. Nahisi magazeti pia hutumiwa kuwajenga hoja zenye kiini macho na kuwazuga wananchi tu – propaganda za kuficha ukweli. Ni kitu cha kufarahisha sana jinsi gazeti la Nipashe la Jumapili 30 Novemba 2008 lilivyoandika kichwa cha habari kikubwa kuwa kampuni ya kimataifa ya wakaguzi wa hesabu wa katika masuala ya majengo M/S Mekon Arc Consult Limited ikishirikiana na kampuni mbili za kimataifa AQE Associates and Bureau for Industries Ltd wameshaanza kazi na wameanza kuuliza maswali kuhusu gharama. Ukweli ni kwamba tenda ya ukaguzi huo – Value for Money, ilikuwa ya ushindani wa kimataifa na makampuni makubwa ya ukaguzi huo wa kitaalamu kutoka nje ya nchi – Africa Kusini, Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda walilita tenda zao lakini wote walipigwa chini kwa kuogopa mambo yasiwe kama yale ya wakaguzi wa EPA. Viongozi wenye hekima serikalini waliopendekeza Ernest & Young wachaguliwe kufanya uchunguzi wa EPA wamelaumiwa vibaya sana na vigogo mbalimbali mafisadi serikarini kwani Ernest & Young waliwashikia bango serikari pamoja ni kupigwa mikwara kibao na kuahidiwa tenda kibao za consulting iwapo wangeisaidia serikali kuficha ukweli. Sasa Governor mpya Ndulu alikuja na moto mkali na nia ya kusafisha Benki lakini mambo yanakuwa magumu na naye kashaonywa asaidie kuzima moto na kufukia mashimo, aibu inatosha.

Kampuniya Mekon Arch Consult Limited inamilikiwa na Mtu anaita Moses Mkony yeye hapo zamani alishakuwa Engineer wa serikalini akipafanyakazi National Housing Corporation. Kwa sasa amestaafu na kufungua kampuni yake hiyo ya Mekon Arch Consult Limited iliyokuwa na ofisi zake sehemu ya Kijitonjama kichochoro cha karibu na shule ya msingi kijitonyama.

Kampuni hiyo imeshirikiana na kitengo cha Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ni kitengo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam chenye kutoa ushauri/consultancy kwa mambo mbali mbali ya ufundi kwa ujumla. Ni mradi wa Chuo Kikuu na sio kampuni binafsi lakini kiongozi wa BICO ni Dr. B.B. Nyichomba. Angalia web page ya BICO katika web site ya chuo kikuu Dar es Salaam

Aqe Associates Ltd pia ni kampuni local ya Quantity Surveyors wako pale Samora Avenue Dar es Salaam,. Tel 255 22 2118225; Tel 255 754 261482 na inamilikiwa na maofisa wa chuo cha Ardhi Institute pale Chuo kikuu, Mmoja wa associates ni Dr. Aldo Lupala mhadhiri pale Ardhi. Hawa ni kuku wa kienyeji mtupu, hakuna hata mzungu wala “ya kimataifa”

Sasa hapo jameni kuna ukweli kuhusu stori ya mwandishi wa Nipashe ya jumapili. Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga hii kampuni na bwana Mkony wanababe wa kukagua Benki kuu kweli. Kipato chao kidogo kabisa, wanawezaje kuwa independent wakati total income yao ni kiduchu na wanataka kukagua benki kuu yenye mabilioni, je code of ethics za Engineers zinakubali hali kama hiyo?

Watakuwa prone for intimidation kani consulting fee toka Benki kuu kwa kazi hiyo ni kubwa mno.

Benki kuu/Gavana kaamua kuchagua kijikampuni kilicho very local, wenyekukimiliki wako hoi kwa poverty wakikimbiza vijitenda vya ujenzi hapa na pale. Kwa makusudi Gavana anataka aweze kuwa–control. Kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango.

Nafikiri ni suala la muandishi wa nipashe kupotosha ukweli aidha makusudi baada ka kula rushwa ya watuhumiwa ili kuanza kuweka kiini macho, au mwandishi kutoku-fanya utafiti wa kina.

Mkitaka kufuatilia ofisi za Mekon ziko wapi, nitawapa picha ya ofisi hizo, ni kujumba kiko Kijitonyama, ukiwa unatokea Makumbusho kuelekea Mwenge, unakata kona ya kushoto ya lami pale Science kuelekea Tandale. Ukiwa barabara hiyo ya Tandale hesabu kona ya tatu kushoto, oposite na car show room moja kata kona hiyo ya kushoto kama uanenda kanisa la KKKT Kijitonyama utaona bango mkono wa kushoto, wanauza makuti ya kusuka, Ukipotea ulizia wanakouza makuti ya kusuka na mafuta ya taa. Ofisi ya Mekon iko hapo. Mekon, Plot 602, Kijitonyama, P O Box 31924 Dar es Salaam, Tel. +255 22 2700784, Fax. +255 22 2647552, Mobile. +255 744 262 249 email
moses_mkony[at]hotmail.com au mekon[at]africaonline.co.tz

Kiini macho hicho cha Gavana Ndulu tumekishutukia. Je kampuni hizo zina utaaalamu wa wa uchunguzi wa kina wa kimahesabu na uwezo wa kugundua wizi wa kalamu?

WANANCHI PASI HIYO, TUENDELEE KUPINGA RUSHWA NA UBADHILIFU WA FEDHA ZA UMMA.

NAOMBA WASOMAJI MUINDELEZE HOJA HII, WANA-NCHI WAPATE UPEO WA SIRI NA VIINI MACHO VYA SERIKARI.

MWANAKIJIJI TAFADHALI IWEKE HII IWE NEWS MPYA YA KUCHANGIA
NIPE EMAIL YAKO NIKUTUMIE DATA/EVIDENCE ZAIDI

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads