Bush arushiwa kiatu cha hasira

Inasemekana kuwa hasira za mwandishi wa habari zilitokana na kuuawa kwa rafiki, ndugu na jirani zake na yeye mwenyewe kusumbuliwa na askari wa Marekani katika mojawapo ya shughuli zake za uandishi. Mwandishi huyo alitamka maneno haya kabla ya kurusha viatu hivyo: "This is a goodbye kiss, you dog"
Kwa mujibu wa wanahabari, katika mila ya KiArabu ni dharau ya hali ya juu kwa mtu kukuonesha soli ya kiatu wachilia mbali kukurushia kiatu chenyewe. Hii ndiyo sababu hasa ya baadhi ya watu kuvua ndala zao na kuikanyaga sanamu ya Saddam Hussein ilipoangushwa.
Mwandishi wa habari huyo na wengine wawili walikamatwa na wana usalama.
Baadhi ya maoni ya watu yanaonesha kukisifu kitendo hicho na kukiita cha kishujaa il hali baadhi ya watu wameshangazwa na kusema hii inaonesha ni kwa kiasi gani upo uzembe katika safu ya ulinzi nchini Iraki.
0 feedback :