wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Friday, November 28, 2008

TweetThis! Tuambizane istilahi za fani mbalimbali

Wakati fulani nimewahi kuandika na kubandika mafundisho ya KiSwahili fasaha kutoka kwa mkufunzi, profesa na sheikh, Ahmed Nabany.

Baadhi ya wasomaji walipenda kupata mawasiliano na mkufunzi huyu hasa zaidi kwa madhumuni ya kupata tafsiri za maneno kadhaa katika fani mbalimbali na mwingine alitaka kufahamiana na babu yake huyo.

Bw. Jackson Muraya, aliye mfuatiliaji, mwanafunzi na msomaji mzuri wa maneno ya KiSwahili ameniandikia ujumbe ufuatao, ambao nauweka hapa aghalabu upate kurejelewa na wengi katika siku za sasa na usoni ili tuweze kuchangishana na kupata maoni zaidi juu ya KiSwahili.

Salamu mwadhamu,
Labda langu pendekezo ni uweke katika blogu yako orodha ya maneno na majina ambayo pia yanahitaji utafiti kama istilahi za Microbiology ili wasomi kufikiria kuhusu sajili kama hizo.
Wakati mwema.
Asante Jackson nitaendelea kuirejea habari hii kadiri nitakavyofanikiwa kuzipata istilahi hizo.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads