wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Saturday, November 08, 2008

TweetThis! Saratani na kilevi vinahusiana

Kila jambo kwa kiasi! Kila kitu kwa wastani!

Matumizi ya kitu chochote kwa binadamu huwa na madhara ikiwa kitu chenyewe hasa kinapokuwa chakula ama kinywaji kitatumiwa kupita kiasi ama kutokutumiwa kabisa. Baadhi ya vyakula na vinywaji si lazima vitumiwe hata kwa kiasi kidogo kwani madhara yake huwa ni makubwa kuliko faida yake. Pia, vipo baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo hadi sasa havijaonekana kuwa na uthibitisho wa madhara yoyote katika afya ya binadamu ikiwa havitatumiwa.

Kutokana na matokeo ya utafifi uliofanywa katika maeneo mbalimbali duniani, imegundulika kuwa saratani ya matumbo ina mahusiano ya karibu kabisa na utumiaji wa kilevi kingi kwa muda mrefu.

Kulingana na utafiti uliofanywa kwa nyakati na maeneo tofauti mfano: Shizuka Sasazuki et al (2002, Japan) pia Song HJ et al, (1993-1998, Korea) na ripoti ya Sandy Dover (2007), muda wa utumiaji wa kilevi ulioonesha madhara ni wa utumiaji wa kilevi mfululizo kwa kadiri ya miaka 18 hadi 24 hivi. Madhara ya kilevi yalionekana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume na baina ya wanawake wenye uzito mkubwa (rejea BMI index zaidi ya 25 huashiria uzito kupindukia) ikilinganishwa na wanawake wenye uzito wa wastani. Madhara hayo huweza kuonekana hata miaka kadhaa baada ya mtu kuacha kilevi.

Sikiliza taarifa ya utafiti (bofya kifute) huo na dalili za ugonjwa wa saratani ya matumbo, kama ilivyoripotiwa na BBC mwaka 2007 mwezi wa Julai.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads