wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, November 13, 2008

TweetThis! Nyumba Ntobhu

MAREJEO:
Kutokana na usumbufu wa baadhi ya wasomaji kushindwa kuona video ya kwanza, nimeongeza video ya pili na baadaye nitaweka ya tatu ili kila mtu awe na uhuru wa kuchagua na kubahatisha itakayoonesha video yenyewe. Samahani kwa usumbufu ninaheshimu miiko ya sehemu za kazi na ni sawa iwe hivyo.
Mila, desturi, tamaduni na kawaida ya maisha hutofautiana kati ya jamii moja na nyingine. Barani Afrika na nchini Tanzania tunayo makabila mengi ambayo nayo yamegawanyika katika koo mbalimbali zenye imani na tabia zinazoshabihiana kwa karibu na kutofautiana sana pia.

Mkoani Mara katika eneo la Musoma, lipo kabila na jamii ambayo mwanamke asiyeolewa lakini aliyejaliwa kuwa na utajiri wa mifugo ama/pamoja na mali, (kulingana na vipimo vya jamii hiyo), anaweza kumtafuta msichana ambaye hajaolewa, akamlipia mahari na hatimaye wakaishi pamoja kwa madhumuni kutunzana na hasa katika hali ya uzee. Utaratibu huu wa kimaisha kwa eneo hilo, wenyeji huuita 'nyumba ntobhu'.

Msichana huyu ambaye amekubali kuishi na mwanamke baada ya kukamlisha taratibu zinazostahili kulingana na na jamii hiyo, yeye atachaguliwa mume na mwanamke aliyemwoa kwa madhumuni ya kupata m/watoto. Pia hutokea ikawa mwanamke aliyeolewa akajadilianana mwanamke aliyemwoa na wakaafikiana kumpa uhuru wa kuchagua mwanaume wa kuweza kuzaa naye watoto.

Watoto waliozaliwa katika 'nyumba ntobhu' huitwa na kuhesabika kwa jina la mwanamke aliyeoa na si mwanaume aliyesababisha uzazi huo.

Tizama video ifuatayo inayoelezea dhana na maisha ya watu wenye 'nyumba ntobhu'.

Utaniuliza, Subi, Je! Huu si ushoga/usagaji?

Nami sitakuwa na jibu. Nipo tayari kusililiza.

Filamu hii imetengenezwa katika mkoa wa Mara, wilaya ya Musoma nchini Tanzania na kudhaminiwa na Maweni Farm


Yatokanayo: Baadhi ya sehemu ya maoni niliyopokea kwenye anwani binafsi:

Mwanamke ambaye hakufanikiwa kupata mtoto yeyote hasa wa kiume anatakiwa amuolee mumewe mke ambaye si lazima awe mke wa mume wake kwa sababu aweza kuwa hata alishafariki ila watoto wote watakaozaliwa na huyu mdada aliyeolewa wataitwa jina la mume wake ili kuendeleza ukoo huo.
Kwahiyo mwanaume yeyote au aliyeteuliwa aweza kumliwaza na kumwezesha kupata watoto.

OR TRY

OR TRY

8 feedback :

marwa said... Thu Nov 13, 03:08:00 AM MST  

i as a people,am delightful for you being inqusitive particulary on this part of kurya custom,but there is also nyumba mboke,where a married womam blessed with no male issues for purposes of inheritance may as well,marry a lady in the same manner as nyumba ntobhu.MARWA,C-MOROGORO

subi said... Thu Nov 13, 03:35:00 AM MST  

Thank you Marwa for the input. I didn't know thet there existed also 'nyumba mboke'. It's always good to hear and learn.

Bishop said... Thu Nov 13, 05:06:00 AM MST  

Mimi si Mkurya ila nimepata kusikia sana mambo haya.

kama ilivyoelezwa kwenye article,nikweli kwamba mama hawa either hawajajaliwa kuzaa ama wamefiwa na waume zao.Na pengine hawakubahatika kuolewa.Huwatolea mabinti warembo mahari(Lobhola)kama ambavyo mwanamume hufanya kwa msichana kisha akaishi naye as her wife ila tu badala ya kumsaga yeye humchukulia wanaume wa kufanya naye tendo la ndoa/ngono na kama akipata ujauzito,kizaliwacho si mali ya yule mwanamume wala yule binti.mtoto ni mali ya mke aliye muweka unyumba mzazi.

Regards;
Bishop

mvungi said... Thu Nov 13, 05:11:00 AM MST  

pamoja na kuwa nmeshindwa kuiona video may be kwa sababu natumia server ya kazini nao wanaprotect watu wadowload sana
bado hii mila naona haikuwa na malice yoyote ile , nadahani mababu ba bibi zetu walikuwa wajanja sana walijua kuwa kama mtu kajaliwa kama hivyo mali au utajiri wowote na bahati mbaya hajawana famila kama mume ana watoto akifa au kuzeeka watu watakuja kumtumnza uizeeni kwa lengo tu la kupata mali zake
hivyo ni katiaka kuandaa mrithi wake anamchagua mwanamke kama hivyo wanakubaliana na anakuwa loyal kwa mchaguzi wake
lakini pia itakuwa ni uonevu kama huyo alochaguliwa hatapata watoto hivyo ili kumpa haki ya watoto anatafutwa mzalishaji ila haki ina baki kwa yule wa awali mwenye mali ili aanze kuapata famila sasa na urithi uendelee na hakuna kukatana mapanga lakini automatically yule baba mzalishaji naye atabenefit

mvungi kiva

subi said... Thu Nov 13, 05:55:00 AM MST  

Nimepata maoni ambayo yamenikumbusha suala la UKIMWI. Jamani ni hivi, bila uaminifu, iwe ni ndani ama nje ya ndoa, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na UKIMWI yapo pale pale. Uaminifu ni jambo la muhimu sana katika maisha! Wala sijui nisisitize vipi. Nikisema hivi nadhani wapo wanaonielewa.
Haya, sehemu ya maoni hayo ilisema hivi:

I think sio usagaji wala Ushoga kwa vile wanawake hao hawana uhusiano wa kimapenzi bali the women anammiliki mwenzake na wakati mwingine anamtafutia mwanaume ili azae.
Kwa kweli kwa wote waliokubali ni kujaribu kukwepa viboko walivyoona mama zao wakipata. At least that is one of the reason I picked up
Ulisikia aliposema hataki udereva..unajua udereva? Umalaya...

Imeonekana lakini kuwa wanawake wa hivi wanaathirika sana na UKIMWI kwa vile wabibi wanakuwa wazee na mara nyingine wanakuwa wanafanya huo umalaya as no permanent relationship yeye anakuwa anazaa tu na bibi anachotaka ni watoto wengi kadri inavyowezekana so wanakufa kweli...

subi said... Fri Nov 21, 12:20:00 PM MST  

Kaka Simon Kitururu anasema:

Kuhusu hili swala la nyumba ya ntobhu, jirani ya kwa bibi yangu mzaa Mama Musoma anafanya hivi. Ila inachojulikana ni kwamba yeye huwa ana maboyfriend na mke wake aliye naye ni yeye humtafutia mabwana.
Kutokana na hilo, nilihisi kuwa wao wawili ingawa mmoja kamuoa mwenzie, hawana mahusiano ya kimapenzi kama ilivyo kwa wasagaji.

Kitu kingine kinisababishacho niamini kuwa katika kuoana kwa mfumo wa nyumba ntobhu ni tofauti na U lezbo, ni jinsi wanavyokufa kwa
UKIMWI. NIliwahi kukutana na mtu ambaye rafikiyake researcher wa mambo ya UKIMWI ambaye ni gay, aliwahi kwenda kujaribu kufanya uchunguzi kuhusu ukimwi kati ya watu wenye uhusiano wa namna hii, akasema mara nyngi katika data alizokusanya alikuta waathiriwa wana strands tofauti za vijidudu vya ukimwi.

Kwa ujumla swala hili silijui sana na mama yangu huaanakwepa kulizungumzia.

Kaka Trio said... Fri Dec 12, 10:28:00 PM MST  

Hi Subi, Naona aidha hutaki kuelewa mantiki ya nyumba ntobhu badala yake umerichi coclusion ambayo kusema kweli haikuwa madhumuni ya ya Nyumba Ntobhu. Mie ni mkurya na nafahamu fika lengo halikuwa kusagana wala umilikaji wa watoto kwa hata siku moja watoto sio mali.

Kwa kikurya nyumba manake ni Nyumba na ntobhu manake ni maskini kwa hivo mtu akiolewa nyumba ntobhu manake ameolewa mahali ambapo kwa namna moja au nyingine palikuwa na mapunufu ya aina fulani. Kinachotokea kwenye nyumba ntobhu ni kwamba yule mama au baba anayetoa mahari aidha ana kuwa hana mtu wa kuja kumrithi na kuendeleza ukoo au hakubahatika kuzaa watoto wa kiume ambao wangeeza kuendeleza ukoo wake. Kwa hivo basi huyo mdada anaeilewa nyumba ntobhu anakuwa sehemu ya familia na anakuwa na haki kama mdada mwengine yoyote ambaye angeolewa ktk familia hiyo.

Kuhusu kuchaguliwa wanaume ninavofahamu hawakuwa wanaenda mahali popote tu kuchagua dume la mbegu. Kama ambavo ulikwisha kujua makabila ya kikrya ni polygamists kwa ivo yule mama au baba ambaye alitoa mahari alikuwa anamuommba mmoja wa ndugu wa karibu wa kiume wa upande wa huko nyumba ntobhu amfanye huyo mdada kuwa mke wake wa kwanza au wapili au watatu au hata wa nne. tena wakati mwengine huyo bwana anaeza kwenda kuchumbia yeye mwenyewe ila mahari ikalipwa na nyumba ntobhu. kuna wangine wadada wanaolewa nyumba ntobhu kisha wanachagua wanyewe wazae na nani. Kwa ufupi lengo nafikiri lilikuwa ni CONTINUITY. Sio usagaji au kumuonea mdada au kuoneza ukimwi. It is unfortunate that kuna ukimwi na poligamists wote wanakuwa hatarini, kuanzia nyumba ndogo hadi dini zengine zinazoruusu kuwa na wake wengi hadi wale maofisa wanaopenda nyumba ndogo.

Tofauti ya wakurya na akina Bill Clintoni na hao watu wa nyumba ndogo ni kwamba wakurya na nyumba ntobhu makes it official!

Kwa taarifa yenu katika makabila mengi ya kikurya kama mdada akizaa kabla ya kuolewa mtoto huwa ni wa mama! kwa hivo haijalishi nani kazaa na huyo mdada mtoto atabaki kuwa wa huyo mdada.

It is what it is, you can't just jump on some peoples custom and culture and start criticizing them without making little research on why why they did what they did. simply because my custom is not similar to somebody else's it does not mean once custom is superior to another. Tell me how and why say CHAGULAGA is better than nyumba ntobhu, Please tell me why nyumba ntobhu culture is so wicked than Tanga's culture of teaching 16 years old girls how to handle a man ( http://mwafrika-kabendera.blogspot.com/2006/12/heaven-on-earth-maidens-made-in-tanga.html ).

nyumba ntobhu by any streach meant no harm to anybody involved. Je kuna wadada wanateswa huko? jibu ni ndio! Je kuna watu wanateseka kwenye ndoa za "kawaida"? jibu pia ni ndio! Hope you are not going to get at me on the issue wives neating, lol.

subi said... Sat Dec 13, 03:46:00 AM MST  

Kaka Trio asante kwa maelezo, ila kama nilivyosema kwenye maelezo yangu ya msingi, mimi nipo tayari kujifunza, suala hili sikuwa na jibu lake na ndiyo nikasema, 'mimi sitakuwa na jibu' kwa sababu sina jibu, basi ya nini niseme uongo kwa nisichokijua? Kwa hivi, yote niliyoandika nimepata maelezo na mawazo ya watu tofauti kama unavyonielezea na wewe pia.
Asante sana kwa maelezo yako.
Habari hiyo ya Tanga sina ufahamu nayo, nalo ni suala jingine nadhani.
Penye wengi kuna mengi!

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads