wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Sunday, November 30, 2008

TweetThis! Baraza la Ushauri kwa Watumiaji Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC)

Baada ya uhuru holela wa baadhi ya makampuni ya mawasiliano na malalamiko yasiyo na idadi kutoka kwa watumiaji wa vyombo vyepesi vya mawasiliano nchini Tanzania, nimefurahi kufahamu kuwa huenda usumbufu na maudhi hayo yakapungua kwa kiasi kikubwa ama taratibu na sheria kuzingatiwa zaidi kufuatia kuanzishwa kwa baraza la utetezi na ulinzi wa haki hizo.

Limeundwa baraza (TCRA-CCC) chini ya Kifungu cha 37 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano namba 12 ya mwaka 2003 kwa mujibu wa sheria za nchi, kwa minajili ya ya kushauri watumiaji huduma za mawasiliano Tanzania.

Muundo: Baraza limeundwa katika kanda saba kulingana na jiografia ya nchi huku kila kanda ikiwakilisha kwenye baraza.

Majukumu: Baraza lina jukumu la kufanya mashauriano katika sekta ya mawasiliano ikiwemo serikali, mamlaka, watoa huduma na makundi mengine.
Baraza lina ruhusa ruksa kutoa na kufuta leseni kwa makampuni ya mawasiliano nchi pale tu inapobidi kufanya hivyo.
Baraza limepewa uwezo wa kuweka viwango vya huduma mbalimbali na kuvisimamia.

Uongozi: Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo ni Bw. Joseph Kessy, anasema kuwa baraza lina wajumbe saba ambao wateuliwa na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.

Utendaji: Baraza limeanza kazi katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara kwa kutetea kwa nguvu maslahi ya watumiaji, kuhamasisha na kuelimisha watumiaji juu ya haki na wajibu wao. Imeundwa kamati kusimamia maeneo haya muhimu: elimu kwa watumiaji na malalamiko, mahusiano na wadau pamoja na utawala, kuandaa utaratibu wa kukutana na wadau pamoja na kusimamia rasilimal za wadau.

Utaratibu wa kuwakilisha malalamiko:  Kuwasilisha malalamiko kwa watumiaji wa huduma ya mawasiliano, walalamikaji wanatakiwa kupeleka malalamiko kwa maandishi kwa mtoa huduma na iwapo hakuridhika atayawasilisha TCRA-CCC.
- Baraza hilo lipo tayari kuwasaidia watumiaji huduma za mawasiliano watakaoathirika.- Walalamikaji wana haki ya kulipwa fidia, kupata taarifa sahihi pamoja na faragha.
- Kila mmoja anawanawajibika kulinda miundombinu, kutunza mazingira na kutoa taarifa.

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads