wavuti.com Updates

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Napenda kuwataarifu kuwa blogu hii inapumzishwa rasmi na tovuti mpya imezaliwa kwa jina www.wavuti.com

This is to inform you that this blog has been retired. A new website to take her place is up and running at www.wavuti.com

Thursday, July 10, 2008

TweetThis! Fedha zenye thamani ndogo duniani

1. Zimbabwe – Mfumuko wa bei ulipofikia kiwango cha 100,000 tu, benki ya Zimbabwe nayo ikafyatua noti yenye sifuri saba, yaani milioni 10 sawa na karibu dola ya Marekani $4 katika soko lisiko rasmi.
2. Vietnam – 500,000- noti ya dong sawa na thamani ya dola ya Marekani $31.37. Katika miaka ya mwanzo ya  1980, Marekani iliiwekea Vietnam vikwazo na hivi kuchagiza gharama za utengenezaji noti za ziada hivyo kushusha thamani ya fedha.
3. Indonesia – 100,000- noti ya rupiah sawa na thamani ya dola ya Marekani $11.05. Mwaka 1997  matatizo ya kifedha katika nchi za Asia yalisababisha Indonesia ipoteze asilimia 80 ya thamani ya rupia yake kwa kipindi cha miezi michache, jambo lililosabajisha maandamano na migomo katika mji wa Jakarta.
4. Iran – 50,000- noti ya rial sawa na thamani ya dola ya Marekani $5.35 tu. Tangu mapinduzi ya mwaka 1979,  mfumuko wa bei nchini Iran umekwea hadi kufikia asilimia 15, wanabahatika tu kutokuendelea kuharibikiwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.
5. São Tomé – 50,000- noti ya dobra sawa na thamani ya dola ya Marekani $3.47 tu. Nchi hii ya Afrika inategemea zaidi manufaa yanayotokana na mauzo yasiyo thabiti na soko la kuyumba la zao la kakao.
6. Guinea – 10,000- noti ya franc yenye thamani sawa na dola ya Marekani $2.33 tu. Mnamo mwaka 2002, nchi hii yenye utajiri wa madini ilitilia ngumu kutekeleza vigezo vya shirika la fedha duniani (IMF)  na ndipo fedha zao za kigeni zilipokauka na kusababisha benki kuu kuchapisha fedha kupindukia hivyo kuishusha thamani yake.
Habari hii imepatikana PortFolio.com

0 feedback :

Recent Comments . Kauli za Wasomaji

###recentComment###

More Opportunities ads